FAIDA 11 ZQ VITUNGUU SWAUMU

Faida 11 za Kitunguu Swaumu katika Mwili

  Kitunguu swaumu ni moja ya viungo mashuhuri duniani. Ingawa wengi wanakula bila kujua kinawanufaishi vipi kiafya katika miili yao. Makala hii imekusanya faida za kitunguu swaumu katika mwili, Utastaajabu jinsi kitunguu swaumu kilivyo na faida tele katika mwili wa binadamu. Siri kubwa inayokifanya kitunguu swaumu kiwe muhimu na faida nyingi za kitabibu ni uwepo wa kampaundi ya Allicin ndani yake.

Kitunguu swaumu kinaweza kutumika katika chakula kama kiungo pia kinaweza kuliwa chenyewe kwa kumeza punje zake zilizosagwa au kunywa juisi yake na kwa matumizi ya katika ngozi hutumiwa kwa kupaka mafuta yake au juisi yake.

 1. Kitunguu Swaumu Huzuia  kuharisha.
 1. Husaidia kupunguza Presha (Hypertension). Kitunguu swaumu kinadhibiti presha kwa kutanua mishipa ya damu na kuzuia kuziba kwa mishipa ya damu.
 1. Kinasaidia kuboresha mfumo wa mmeng’enyo wa Chakula. Kutumia kitunguu swaumu katika chakula inasaidia kuboresha mmeng’enyo wa chakula, na hata uvimbe au maumivu yaliyopo katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula yanaweza kutulizwa kwa kitunguu swaumu.
 1. Kitunguu swaumu kinadhibiti Kisukari. Mafuta yanayotokana na kitunguu swaumu yana uwezo wa kumsaidia mgonjwa wa Kisukari asipate matatizo yanayoweza kusababishwa na kisukari kama matatizo ya moyo, madhara katika figo na kudhoofisha mfumo wa fahamu.
 1. Husaidiakutuliza maumivu ya sikio. Kitunguu swaumu kina uwezo wa kupambana na virusi, fangasi (fungus) na bakteria. Mafuta ya kitunguu swaumu huchanganywa na mafuta ya Mzaituni ka kuwekwa katika sikio linalouma.
 1. Husaidia kuzuia kansa (saratani). Kula kitunguu swaumu mara kwa mara husaidia kuzuia kansa ya koo, utumbo mpana na tumbo. Kitunguu swaumu huzuia uzalishaji wa kampaundi za Kasinojeni (Carcinogenic Compound) na kuzuia kutokea kwa uvimbe.
 1. Kitunguu swaumu huzuia chunusi. Kitunguu swaumu kikichanganywa na asali na kupakwa sehemu yenye makovu ya chunusi huyaondoa kabisa na kuzuia kurudi kwa chunusi.
 1. Husaidia kudhibiti Kifua cha Pumu (Asthma). Punje za Vitunguu swaumu zilizochemshwa zina msaada mkubwa katika kudhibiti Kifua cha Pumu (Asthma). Kwa mtu mwenye matatizo ya Pumu, Kila siku kabla ya kulala anywe glasi ya maziwa na punje tatu za Kitunguu swaumu zilizochemshwa itamsaidia sana kuboresha afya yake.
 1. Huongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa. Kwa wanandoa ambao hukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa watumie kitunguu swaumu kitawasaidia sana. Na hii ni kwa wote mwanamke au mwanaume.
 1. Husaidia kupunguza lehemu (cholesterol) mwilini. Lehemu nyingi katika mwili inaweza kusababisha kuziba kwa mishipa ya damu na kupelekea matatizo ya moyo na presha. Njia rahisi ya kuondoa lehemu mwilini ni kwa kutumia kitunguu swaumu kwa kuchanganya katika mlo wako kila siku.
 1. Husaidia kutibu vidonda. Kamua punje za vitunguu swaumu na utumie juisi yake kupaka sehemu yenye kidonda.

Zingatia: Ongeza matone mawili hadi matatu katika kiasi kidogo cha juisi ya kitunguu swaumu kabla hujapaka katika kidonda. Kupaka juisi tupu bila ya kuongeza matone ya maji kunaweza kusababisha muwasho.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *