Massage huondoa maumivu ya hedhi

Massage ni Suluhisho la maumivu wakati wa hedhi

Hedhi ni hali ya kimaumbile inaysojitokeza kwa wanawake waliopevuka (waliofikia balehe). Katika kipindi hiki wanawake hutokwa na kiasi cha damu kwa muda kati ya siku 3 hadi 7.

Damu hutoka baada ya yai liliozalishwa kutoka katika ovari kukosa mbegu ya kiume ya kulirutubisha. Hivyo kuta za mji wa mimba ambazo ziliandaliwa kimaumbile kwa ajili ya kubeba mimba hukwanguliwa na kutoka nje ya mwili kupitia mlango wa uzazi wa mwanamke kama damu chafu na nzito.

Katika kipindi cha hedhi au siku chache kabla wanawake wengi hupata maumivu chini ya kitovu na wengine katika mgongo na sehemu za nyonga.

Sababu za Maumivu wakati wa hedhi

1.Kukwanguliwa kuta za mji wa mimba (uterus). Tishu laini zilizojaa damu katika kuta za mji wa mimba hukwanguliwa baada ya yai kukosa mbegu ya kiume ya kulirutubisha. Kitendo hicho husababisha maumivu katika eneo hilo la mji wa mimba na hapo ndipo mwanamke anahisi maumivu ya tumbo.

2.Kutanuka kwa misuli ya mji wa mimba: Wakati misuli ya mji wa mimba inatanuka kwa ajili kusukuma damu itoke nje ya mji wa mimba mwanamke aliyopo kwenye hedhi hupata maumivu makali.

3.Kiwango kidogo cha damu katika mji wa mimba: kemikali ya prostaglandin huzuia damu isifike kwa wingi katika mji wa mimba. Hali hiyo pia husababisha na oksijeni kupungua katika eneo hilo.

4.Kemikali ya prostaglandin hufanya ncha za neva ziwe kali kwa kuhisi maumivu hivyo mtu hujisikia maumivu zaidi.

5.Pia kukosekana kwa kiwango kikubwa katika mji wa mimba wakati wa hedhi husababisha maumivu.

Jinsi Massage inavyosaidia kuondoa maumivu wakati wa hedhi

Massage ambayo hufanyiwa mtu mwenye maumivu wakati wa hedhi inalenga maeneo muhimu yanayohusika kama tumbo, mgongo, mapaja na katika nyayo.

Massage husaidia kuondoa maumivu wakati wa hedhi kwa sababu;-

1.Massage huongeza mzunguko wa damu eneo ambalo linafanyiwa massage. Hivyo uwepo wa kiwango kikubwa cha damu katika eneo la mji wa mimba huongeza oksijeni na kupunguza maumivu.

2.Massage husababisha kuzalishwa kwa vituliza maumivu vya asili (natural pain killers) kutoka katika ubongo. Hivyo maumivu huondolewa katika eneo linalofanyiwa massage.

3.Kuongezeka kwa homoni za serotonini na endophirn: Hizi ni homoni za furaha ambazo humfanya mtu ajisikie mtulivu na mwenye furaha, pia hupunguza maumivu. (Mayo Clinic).

Hivyo massage ina uwezo mkubwa wa kuondoa maumivu wakati wa hedhi

Hitimisho

Maumivu wakati wa hedhi yanatokana na sababu mbalimbali ikiwemo na zilizotajwa hapo juu. Kama mtu anapata maumivu kutokana na matatizo mengine ya uzazi anatakiwa apate ushauri kwanza kutoka kwa Daktari kabla hajaanza kufanyiwa massage,

Suluhisho

Kama wewe ni muathirika wa tatizo hili unaweza kufika katika kutuo chetu cha Happiness Massage Clinic kilichopo Lamada Hotel, Apartment no. 27, Ilala Dar es Salaam kwa ajili ya ushauri na huduma ya massage. Unaweza kutupigia simu Namba: 0715343161.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *