BEST BODY SCRUB SERVICE

Faida 10 za SCRUB Katika Ngozi

`1. Huondoa seli mfu katika ngozi

Seli za binadamu zilizopo katika ngozi zinakufa na huendelea kubaki zikiwa zimeshikamana na seli nyingine katika ngozi. Idadi ya seli hizi inapoongezeka husababisha kufifia kwa mwonekano halisi wa ngozi na pia huweza kusababisha hata kuziba kwa baadhi ya matundu ya jasho kwani hugeuka kuwa uchafu. Kwa kuwa si rahisi kuondoa seli mfu kwa kuoga kwa kawaida, Scrub yenye mchanganyiko wa karafuu, kitunguu swaumu, mdalasini na manjano ina nguvu kubwa ya kuondoa seli mfu na kuboresha afya ya ngozi yako.

2. Hung’arisha ngozi na kuifanya iwe na mwonekano unaovutia

Nguvu kubwa ya kung’arisha ngozi iliyopo katika manjano imeongezewa nguvu zaidi na viambata vingine ambavyo vina uwezo mkubwa wa kuifanya ngozi yako iwe nyororo na yenye mvuto.

3. Huboresha afya ya ngozi kwa ujumla

Uwepo wa vitamini C, E na K katika mchanganyiko wa scrub hii ina uwezo mkubwa wa kuboresha afya ya ngozi yako na kukufanya uwe salama zaidi katika mazingira. Ngozi ni ogani kubwa katika mwili wa binadamu ambayo inaufunika mwili wako wote na kuukinga na vitu mbalimbali. Ngozi ina kazi ya utoaji takamwili, kurekebisha joto mwilini, kukinga sehemu za ndani za mwili pamoja na kukujulisha hali mbalimbali za mazingira kama vile upepo, joto na baridi na miguso. Hivyo kuwa na ngozi yenye afya nzuri sio jambo la muhimu tu bali pia ni lazima.

4. Kuondoa mikunjo ya ngozi na kupunguza kasi ya kuzeeka.

Scrub yenye mchanganyiko wa kitunguu saumu, manjano, mdalasini, kahawa na karafuu ina ufanisi mkubwa wa kuondoa mikunjo ya ngozi  hata kwa  wanaozeeka na hivyo hupunguza kasi ya kusinyaa au kukunjana kwa ngozi kwa watu wenye umri mkubwa.

 

5. Hutibu chunusi na madoa katika ngozi

Karafuu na kitunguu swaumu vilivyomo katika scrub hii ni tiba nzuri kwa chunusi na madoa katika ngozi. Kahawa pia ina nguvu kubwa ya kuondoa mabaka meusi katika ngozi na kuing’arisha.

 

6. Hukinga ngozi dhidi ya maambukizi ya fangasi na bakteria

Ngozi hushambuliwa na vijidudu kama bakteria na hasa hasa fangasi. Scrub hii ni tiba nzuri kwa kutibu athari au mashambulizi ya fangasi na bakteria, pia huweka ulinzi dhidi yao. Hivyo ngozi inayofanyiwa scrub yenye mchanganyiko wa kitunguu saumu, manjano, mdalasini na karafuu ni vigumu kushambuliwa na bakteria au fangasi.

 

7. Kinga dhidi ya uvimbe katika ngozi

; Manjano iliyopo katika scrub hii imeboreshwa kwa kuongezewa viambata vingine vitatu ambavyo vinaipa nguvu zaidi ya kukinga uvimbe unaotokea katika ngozi kwa sababu za kibailojia kama vile bakteria.

 

8. Hulainisha ngozi kavu.

Ngozi iliyo kavu inakosa ufanisi katika utendaji wake na hivyo ni rahisi kusababisha madhara katika mwili. Kwa kutumia scrub hii ina uwezo wa kulainisha ngozi na kufungua vizuri vinyweleo vilivyopo katika ngozi.

 

9. Hukinga ngozi kutokana na saratani.

Virutubishi na atioxidants vinavyopatikana katika scrub hii vina nguvu kubwa ya kuikinga ngozi dhidi ya saratani (skin cancer).

10. Huondoa mikunjo kwa watu wanene (cellulite):

Scrub hii ina ufanisi wa hali ya juu katika kuondoa mikunjo ya ngozi kwa watu wanene. Mikunjo hii mara nyingi hutokea sehemu za matako na mapajani ingawa inaweza kutokea pia katika sehemu nyingine za mwili. Mikunjo hii husababishwa na mrundikano mkubwa wa mafuta chini ya ngozi.

KWA MSIMU HUU WA OFA UTAFANYIWA BODY SCRUB KWA TSH 20,000/= TU

TUPIGIE SASA KUWEKA NAFASI YAKO

0715343161

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *