KUPASUKA VISIGINO

Mipasuko katika Visigino: Sababu, Athari na Suluhisho lake

Kuwa na miguu au visigino vilivyopasuka (magaga au machacha) ni moja ya sababu inayoweza kuonyesha kuwa katika mwili wako kuna upungufu wa virutubisho kadhaa, vitamini au madini.

Japo wengi wetu tumekuwa na mitazamo kwamba, visigino kupasuka ni ishara ya mtu kutojali usafi wa miguu yake, ila  leo napenda kukushirikisha mambo kadhaa kuhusu mtu kupasuka visigino.

Kwa kawaida, ngozi zetu huwa zina unyevunyevu ambao huiwezesha ngozi ivutike au kutanuka pamoja na kusinyaa bila ya kutokea madhara yoyote kama vile kuchanika.

Pamoja na ngozi kugawanyika katika sehemu tatu ( sehemu ya nje – Epidermis, sehemu ya kati – Dermis na sehemu ya ndani –  Endodermis), ni sehemu ya nje, epidermis, ambayo ipo karibu na unaweza kuigusa au inaweza kuathirika na ukaiona kirahisi, na hii ni kwa sababu inagusana moja kwa moja na mazingira yetu. Magaga huanza hutokea katika sehemu hii ya ngozi, Epidermis.

Sababu zinazopelekea Visigino kuchanika / kuweka nyufa (Magaga)

Miongoni mwa sababu zinazoweza kumfanya mtu kupasuka au kuweka nyufa visigino ni pamoja na:

1.Ngozi kuwa kavu sana

hii ni sehemu ya nje ya ngozi ambayo inawezekana mtu kwa asili yake akawa na ngozi kavu na hivyo kuifanya ishindwe kustahimili kutanuka au kusinyaa na hivyo kupelekea nyufa au mipasuko katika visigino.

2.Kuiweka miguu katika maji kwa muda mrefu

Hali hii husababisha ile asili ya ngozi pamoja na mafuta katika ngozi yapotee na kuiacha ngozi ikiwa kavu sana, hivyo hupelekea mipasuko katika visigino kwa urahisi.

3.Kuwa na uzito mkubwa

Hali hii husababisha presha kubwa iwe katika miguu unapokanyaga na endapo ngozi yako haitokuwa na uimara wa kutosha itasababisha visigino vipasuke.

4.Upungufu wa virutubisho.

Upungufu wa Vitamini, madini na zinc katika mwili husababisha afya dhaifu ya visigino na hivyo ni rahisi kupata mipasuko.

Athari za Kupasuka Visigino

Mipasuko ya visigino ina mwonekano usiovutia na hii ndio kero kubwa kwa watu wengi, lakini pia wakati mwingine inaweza kusababisha maumivu ukitembea.

Kutokana na mipasuko hiyo vilevile mtu anaweza kupata maambukizi ya fangasi na bakteria kwa urahisi na hivyo kuwa katika hatari ya kupata magonjwa mengine. Unashauriwa kupata suluhisho la haraka pindi utakapoona una magaga katika visigino kwani yatapatiwa suluhisho sahihi kwa urahisi zaidi.

Suluhisho na kupasuka kwa visigino

Suluhisho bora kabisa la kupasuka kwa miguu linapatikana baada ya kujua sababu ya kupasuka kwa miguu. Hivyo  Happiness Massage tupo kwa ajili yako kukupatia suluhisho kamili la tatizo lako la kupasuka miguu.

Tunakupatia ushauri wa jinsi ya kula vizuri na tuna mafuta maalumu ambayo yanaweza kulainisha nyayo zako ndani ya siku chache tyu baada ya kuyatumia.

APRICARE 3

 

Tupigie simu 0715343161 au Fika ofisini, Lamada Hotel, Ilala Dar es Salaam. Happiness Massage, Tunarejesha Furaha Yako.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *